Mjasiriamali na Ujasiriamali

Sifa za Mjasiriamali

Mjasiriamali ni mtu wa aina gani? (Sifa za Mjasiriamali)

 

 

  • Ni mtu ambaye anaanzisha na kumiliki biashara
  • Ni mtu ambaye yupo tayalia kuthubutu
  • Ni mtu ambaye ni mbunifu
  • Ni mtu jasiri asiyeogopa kushindwa
  • Ni mtu ambaye kila siku anatafuta njia mpya za kuzalisha na kuleta  mabadiriko mapya
  • Ni mtu mvumilivu
  • Ni kiongozi
  • Ni mshindani asiyekata tamaa
  • Ni mtu ambaye anapenda kuwajibika na anafanya kazi kwa bidii
  • Ni mtu anayetazama maisha ya mbele
  • N mtu ambaye anaweza kubadirisha na kutumia nafasi kama fulsa. 
  • Ni mtu ambaye anahitaji na anahamu ya kupata mafanikio
  • Ni mtu ambaye anaweza kujitegemea.

 

Je wewe unasifa hizo hapo juu? Hata kama hauna sifa zote zilizoorodheshwa hapo juu, bado unaweza kuwa Mjasiriamali.

Chanzo: http://gjobu.blogspot.com/2012/04/dhana-na-asili-ya-ujasiriamali.html (Mwandishi: George Jobu)

Faida katika Ujasiriamali

Zifuatazo ni baadhi ya faida ambazo zinatokana na ujasiriamali

  1. Ujira binafsi na nafasi za ajira kwa watu wengi
  2. Kupunguza umasikini miongoni mwa watu
  3. Kutumia ipasavyo rasilimali tulizonazo
  4. Matumizi sahihi ya rasilimali watu
  5. Ujasiamali hutupa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughuri mpya
  6. Kukuza na kuendeleza uchumi katika nchi
  7. Kupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa watu
  8. Kupunguza tofauti katika maendeleo baina ya watu, mikoa, nchi n.k

Mjasiriamali anajengwaje?

Vitu vinavyomjenga mjasiriamali ni pamoja na vifuatavyo:

FULSA
Fulsa ni kama uti wa mgongo kwa mjasiliamali. mjasiliamali lazima awe na uwezo wa kutambua au kugundua fulsa, uwezo wa kuchambua na kuchanganua fulsa pia kuchukua hatua juu ya fulsa husika.

MTAJI
ni kitu chochote ambacho mjasiliamali anawezatumia katika kuzalishia au kufanyia jambo flani kwa lengo la kupata faida. mtaji umegawanyika katika miundo ifuatayo:- mtaji wa fedha,nguvu kazi,mtaji jamii,elimu na utaalamu katika jambo flani.


UBUNIFU
Kwa kawaida mjasiliamali anatakiwa kuwa mbunifu, ubunifu ndio unamtofautisha mtu mmoja na mwingine hata kama wote watafanya jambo linalo fanana. kilasiku unatakiwa kufikili ni jinsi gani utafanya jambo jipya ua jambo lililofanya na wengine lakini wewe ufanye katika njia tofauti.

MAWASILIANO
Mawasiliano huunganisha vitu pamoja ana huweka watu pamoja na husaidia kupata taarifu huhimu  katika biashara yako.Mawasiliana huunganisha mtaji, fulsa na ubunifu, mjasiliamali anatakiwa kuboresha mawasiliano ili afanikiwe katika ujasiliamali wake.

Tovuti ya Mjasiriamali

Tovuti ya Mjasiriamali ambayo itakuwa inapatikana katika anuani hii www.mjasiriamali.co.tz ina malengo yafuatayo:  

  • Kutoa Taarifa na Elimu ya Ujasiriamali kwa watu wote mahali popote Tanzania
  • Kuchochea Ujasiriamali na kuongeza Maarifa kwa mjasiriamali mmoja mmoja
  • Kuwatangaza Wajasiriamali na kazi zao
  • Kuwaunganisha Wajasiriamali na wadau wengine
  • Kuwasaidia Wajasiriamali kuuza bidhaa zao

Unaweza kuwa mjasiriamali !

Mambo mengi sana yanasemwa, yamesemwa na yataendelea kusemwa kuhusu ujasiriamali na wajasiriamali.  Wengi wamefanikiwa. Wamepita katika changamoto nyingi lakini hawakukata tamaa. Wengine, mafanikio yao yamebadilisha dunia kabisa na majina ya biashara zao ndio umekuwa wimbo katika midomo ya watu wengi.

Biashara za wajasiriamali , tena zilizofanikiwa, zimeanzishwa na wajasiriamali wa kila aina. Kila mtu ana hadithi yake na njia yake. Sio kwamba wote wamepita katika njia moja. Hapana! Wapo waliosoma sana, wapo ambao hawajasoma sana na wapo ambao wamesoma kidogo sana. Wengine hawakumaliza shule zao, bali waliishia katikati. Wengine walisoma kwa kiwango kikubwa kabisa. Lakini wote hawa, pasipo kutegemea walikotoka, ni wajasiriamali waliofanikiwa. Wote waliziona fursa, wakazichangamkia na sasa wamefanikiwa.

Baadhi ya wajasiriamali wamekuja na mawazo makubwa kabisa na ubunifu mwingi hata kuanzisha miradi, shughuli na biashara ambazo zimebadili jamii kabisa. Wapo ambao hugundua fursa baada kufanya utafiti wa kina katika mambo, wakitafakali kwa kina wachukue hatua gani sahihi na hata wakihusisha wataalamu mbalimbali katika kuwasaidia.

Lakini pia wapo wajasiriamali ambao wanapopata wazo la biashara , wanalirukia, wanakwenda nalo kama lilivyo na mambo mengine yatajijua mbele ya safari.

Mtu yeyote yule anaweza akafanikiwa katika biashara kama mjasiriamali. Hakuna sifa ya aina moja ambayo ndiyo kama kanuni inayotakiwa ili mtu afanikiwe kama mjasiriamali.

Je ni nini kinakuzuia usifanye ujasiriamali na kuwa mjasiriamali aliyefanikiwa? Endelea kutembelea tovuti ya mjasiriamali.co.tz maana unaweza kuwa mjasiriamali!